BREAKING NEWS: NGULI WA BARCELONA ‘CRUYFF’ AFARIKI KWA KANSA
Mchezaji wa zamani wa Uholanzi na vilabu vya Fc Barcelona na Ajax JOHAN CRUYFF amefariki mapema leo akiwa na umri wa miaka 68 kwa tatizo la Cancer.
Cruyff alijijengea jina lake akicheza kama mshambuliaji kwenye timu ya uholanzi na Barcelona na amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or
Alichukua ubingwa wa ulaya mara tatu mfululizo akiwa na Ajax kisha akahamia na akafanikiwa kuwapa Barcelona ubingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza mwaka 1992.
Pia aliifikisha timu yake ya Uholanzi kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 1974 na walifungwa na Ujerumani.
Mwezi wa pili mwaka huu Johan aliwaita wachezaji wa Barcelona na kuwambia juu ya hali yake mbaya na kuwahakikishia kuwa atakufa muda si mrefu hivyo wajitahidi kushinda kila kitu kama alivyofanya yeye na Rais wa Barcelona aliahidi klabu itamuenzi kwa mazuri yote aliyoifanyia
Cruyff ndiye aliyeifundisha Barcelona falsafa yake ya pasi nyingi na hadi sasa wanaitumia na wamefanikiwa kuwa moja ya vilabu bora sasa duniani.
Ulimwengu wa soka March 24 2016 umepata taarifa za msiba wa nguli wa soka waUholanzi aliyewahi kuvichezea vilabu vya Ajax na FC Barcelona ya Hispania Johan Cruyff. Nguli huyo ameripotiwa na BBC Sport kufariki kwa kansa leo akiwa na umri wa mika 68.
.
Johan Cruyff pia aliwahi kuja Tanzania na kumpatia zawadi ya jezi rais mstaafu wa awamu ya nne DK Jakaya Kikwete
Hapa alikuwa akimkabidhi zawadi ya jezi Rais Shein wa Zanzibar,
Kama hukuwahi kupata bahati ya kushuhudia uwezo wa Johan Cruyff, video ina majibu yote.
Post a Comment