Header Ads

KUPATWA KWA MWEZI USIKU WA IJUMAA KUANZIA SAA 4 USIKU.

        Image result for lunar eclipse
Kupatwa kwa Mwezi ni tukio linaloweza kutazamwa kutoka sehemu kubwa ya dunia na linaweza kushuhudiwa kwa wakati mmoja na mamilioni ya watu muda ule ule wakati tukio linapotokea angani. Kwa hiyo tukio hili linachukuliwa kama ni la kawaida na kuchukuliwa kama tunavyochukulia kuchomoza kwa Mwezi. Kwa upande mwingine, kupatwa kabisa kwa Jua huaonekana katika ukanda mwembamba tu wenye upana wa kiasi cha kilomita 100 hivi. Hivyo idadi ndogo sana ya watu wamewahi kuona Jua likipatwa kabisa na kuwa kiza kama usiku pamoja na anga ya moto inayozunguka Jua.

Tukio la kupatwa kwa Mwezi litakalotokea Jumamosi hii, tarehe 10 Desemba.  Ni tukio muhimu kwa nchi yetu kwa vile ni mwanzo wa kipindi kingine cha miaka 50 ya uhuru wetu. Pamoja na hiyo, tukio Jumamosi hii litashuhudiwa na watu wachache sana duniani. Mwezi utaonekana umepatwa kabisa katika bara la Asia tu.  Hapa Tanzania Jumamosi hii, sisi tutaona mwisho tu wa kupatwa kwa Mwezi.  Wakati wa magharibi, wakati Jua likizama, ukiangalia upande wa mashariki utaona Mwezi Mpevu ukichomoza, na nusu ya sura ya Mwezi itakuwa imefunikwa na kivuli kizito cha Dunia.

Baada ya tukio la mwisho la kupatwa kabisa kwa Mwezi lililotokea tarehe 15 Juni mwaka huu na kuficha kabisa sura ya Mwezi, kupatwa tarehe 10 Desemba itatokea upeoni na nusu tu ya sura itafichwa. Pia kutakuwa na tofauti kubwa katika kiasi cha kupatwa kitakachoonekana sehemu mbalimbali za Tanzania. Wale wanaoishi upande wa mashariki wa nchi wataona sehemu kubwa ya kupatwa huko kuliko itakavyoonekana upande wa magharibi mwa nchi.

Katika kanda ya pwani, Mwezi Mpevu utachomoza saa 12:33 jioni baada ya Jua kuchwa saa 12:27 jioni. Wakati huu, nusu ya juu-kushoto ya Mwezi itakuwa imefunikwa na kivuli cha Dunia. Mwezi utaendelea kupanda wakati kivuli nacho kinapotea polepole. Kupatwa kutakapokwisha saa 1:18 usiku, Mwezi utakuwa umepanda kiasi cha nyuzi/digrii 10, kwa hiyo watu wengi wa ukanda wa mashariki wataweza kuona kupatwa huko alimradi upeo wa mashariki usiwe na mawingu au kipingamizi kingine. Ikiwezekana, chagua mahali ambapo upeo wa mashariki unakuwa wazi kabisa, kwa mfano sehemu ya pwani, na utakuwa miongoni mwa watu wachache watakaobahatika kuangalia tukio hili adimu.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.