YOUNG DEE AMEFUNGUKA HAYA BAADA YA DOGO JANJA KUMDISS...........
DOJO JANJA
Baada ya Hitmaker wa My Life Dogo Janja kufunguka kuchukizwa na msimamo wa rapa Young Dee kuhusu video aliyoipost meneja wake Babu Tale akiwa na msanii mkongwe Chid Beenz, Young Dee amesema hajalishwi na maneno ya Dogo Janja.
POST YA BABU TALE AKIWA NA MSANII CHID BENZ
Kupitia kipindi cha Planet Bongo East Africa Radio Young Dee amesema ameshazoea maneno hasi (Negative) kutoka kwa watu hivyo siku hizi hayamshtui na wala hajali chochote kuhusu maneno hayo.
YOUNG DEE
Kuhusu tuhuma za kutumia madawa ya kulevya Young Dee ameendelea na msimamo wake ule ule kuwa hatumii madawa bali ni fununu tu zinazozushwa juu yake.
POST YA DOGO JANJA
Hata hivyo alivyoulizwa kuhusu post ya Dogo Janja ya kumdiss alisema hajaiona,hafatilii na hayo ni mambo negative ambayo huwa hapendelei kuyapa kipaumbele.
Post a Comment