Header Ads

MATUMIZI YA SIMU FEKI YAMEANZA KUPUNGUA-DKT.SIMB

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Dkt. Ally Yahaya Simba amesema asilimia 40% ya simu hapa nchini ni feki ndiyo maana wametoa muda wa miezi 6 kuanzia Januari mwaka huu hadi Juni ili wananchi waweze kutafuta simu zenye ubora.




Dkt. Simba ameyasema hayo alipokuwa akizunguzungumza katika kipindi cha East Africa Drive kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa ambapo amesema kuwa lengo la kufanya kampeni ya kuondoa simu feki sii la kutenganisha kati ya matajiri na maskini bali ni kuwa na simu zenye viwango vinavyotakiwa katika matumizi salama.
''Kuna simu unaweza kununua milioni 2 lakini ikawa feki lakini mwingine akanunua simu yake ya shilingi elfu 30 au 40 na ikawa 'original' hivyo jambo la msingi ni wananchi kuhakikisha simu wanazonunua kabla ya kutoka dukani wahakikishe simu ni salama kwa kubonyeza *#06# utaletewa kitu kinaitwa IMEI hizo namba zitume kwenda namba 1509 utapata majibu kama simu yako inatambullika au la” Amesema Dkt. Simba
Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kampeni ambayo inaendelea ya kubaini simu feki utafiti ulionyesha asilimia 40% ya simu zilikuwa feki ila sasa watu wameanza kuzibadilisha hadi imefikia asilimia 18% hali ambayo inaashiria wananchi wanamwitikio katika kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa.
Wakati huo huo Dkt. Simba amesisitiza kuwa wananchi wafahamu kwamba wakikosewa katika mitandao ya kijamii hatua ya kwanza ni kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ndipo hatuo nyingine za kisheria zitafuata na TCRA haishughuliki na kesi za mitandao ambazo hazijaripotiwa kwanza polisi.

.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.