Alifahamika kama mkali wa kuchana na Free style za kutosha miaka ya nyuma na hakuna aliyefikiri angeweza kugeuka na kutengeneza hitsong kwa kuimba 100%.
Inaitwa Kwetu ni ngoma ambayo kaitambulisha juzi tu lakini matokeo yake ni kubwa kwasasa kutokana na maudhui yake yaliyolenga maisha ya vijana wengi wenye kipato duni, nyimbo hiyo imetokea kupendwa na watu wengi.
Ni msanii Raymond ambaye amefunguka kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio na kuweka wazi kuwa yeye alikuwa msanii wa kurap lakini hakuwa mwanaharakati wa Hip Hop kwasababu Hip Hop ukiifanya kama dini itakutesa.
Raymond amezidi kueleza kuwa wapo watu ambao ni wanahip hop na hawafanyi rap kwahiyo Muziki wa hip hop siyo Dini kwahiyo ameamua kuimba kwa kuona anaweza kufanikiwa kulingana na uwezo wake na ushauri wa menejimenti yake ya WCB.
Hata hivyo ameweka wazi kuwa kipaji chake cha kurap bado kipo na ana nyimbo kibao alizorap zipo na kila akipata mizuka ya kurap huwa anaandika mistari na kuitunza.
Msanii Raymond anasifika pia kwa uwezo wake wa kuandika, sifa ambayo ni kigezo kikuu kwa msanii kuingia WCB kwa mujibu wa Babutale na msanii Diamond Plutnumz.
Post a Comment