AGIZO JIPYA KUHUSU USAFI SIKU YA JUMAMOSI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.
Watanzania Wenzangu mtakumbuka kwamba tulikubaliana tuwe tunafanya usafi wa mazingira yetu nchi nzima kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuitikia wito wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliouanzisha tarehe 09 Desemba 2015.
Nachukua nafasi hii kuwasihi Watanzania wote kushiriki kikamilifu kufanya Usafi wa Mazingira kwenye Makazi yetu, Maeneo yetu ya Biashara, maeneo ya Taasisi za Umma na maeneo yenye mikusanyiko ya watu mbalimbali kama masokoni na minadani.
Mbali ya kwamba kufanya usafi kuna fanya mazingira yetu yapendeze na hivyo kuondoa magonjwa yanayo sababishwa na uchafu lakini pia zoezi la kufanya usafi kwa pamoja lina jenga Umoja na Mshikamano wa kitaifa, linaondoa matabaka ndani ya jamii yetu. Natoa wito kwa kila Mtanzania Kujitokeza kufanya usafi bila kujali uwezo wa mtu,hadhi yake,cheo chake, au nafasi yake katika jamii. Viongozi wa makundi yote katika jamii tuwe mfano katika jambo hili jema.
RAIS JOHN JOSEPH MAGUFULI
AKIFANYA USAFI WAMAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM
Post a Comment