Header Ads

MALAIKA AFUNGUKA KIASI ALIOTUMIA KUJENGA NYUMBA YAKE .

Msanii wa kike ambaye anafanya muziki wa Bongo Fleva, Malaika amefunguka kiasi alichotumia kujenga nyumba yake mpya.
malaika-2
Nyumba ya Malaika anayoijenga
Hitmaker huyo ‘Zogo’ amekiambia kipindi cha Ujenzi cha East Africa TV kuwa nyumba hiyo imemgharimu kiasi cha shilingi milioni 30 mpaka sasa ilipofikia ambapo kwa zaidi ya asilimia 90 imeshakamilika. Hizo ni gharama nje ya kiwanja.
Malaika ameongeza kuwa familia yake ndiyo iliyochangia yeye kujenga nyumba hiyo kwa kuwa walimshauri mapema kufanya hivyo kabla hajaachana na mpenzi wale ambaye pia alikuwa akimsimamia kazi zake za muziki.
Alisema kuwa hakuamini kwa kidogo alichokuwa anapata angeweza kujenga nyumba yake na ikakamilika. Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake ‘Rarua’ uliotoka April, mwaka huu.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.