EXCLUSIVE;- MUIGIZAJI HAJI JUMBE ( Mr. Benson) WA TAMTHILIA YA SIRI ZA FAMILIA AFARIKI.
Muigizaji Haji Jumbe, ambaye amekuwa akiigiza kama Mr. Benson katika tamthilia ya Siri za Familia inayorushwa na EATV amefariki Jumatatu jioni katika Hospitali ya Kinondoni kwa Dr. Mvungi. Siku chache zilizopita alikuwa anasumbuliwa na tumbo.
Mazishi yanatarajia kufanyika Jumanne saa 9 Alasiri, huko Bagamoyo, Pwani.
Marehemu Haji Jumbe kwa jina la usanii Mr. Benson
Post a Comment