Ben Pol: SI LAZIMA KUMSHIRIKISHA MTU ILI WIMBO UWE MKUBWA.
Mkali wa muziki wa RnB, Ben Pol amefunguka sababu inayoweza kuufanya wimbo ukawa mkubwa.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa wimbo ukiwa mzuri ni rahisi kuhit hata usipomshirikisha msanii mkubwa.
“Kinachoboost wimbo si msanii bali ni wimbo wenyewe. Ukiangalia ‘Moyo Mashine’ nimeimba mwenyewe umekuwa mkubwa, ‘Sofia’ niliimba mwenyewe lakini wimbo ulikuwa mkubwa sana,” amesema Ben.
Ben Pol ameongeza kuwa kuwashirikisha wasanii wenye majina makubwa hakufanyi wimbo ukapendwa zaidi ila ufundi uliotumika kwenye wimbo wenyewe ndio utaufanya wimbo huo kupendwa. Kwa sasa wimbo wa ‘Moyo Mashine’ umeendelea kufanya vizuri kwenye redio na TV japo una zaidi ya miezi mitano tangu utoke.
Post a Comment