CHECK DIAMOND PLATNUMZ NA CASSPER NYOVEST KWENYE COLLABO MOJA NDANI YA COKE STUDIO NDANI YA SOUTH AFRICA .
Diamond na Cassper Nyovest rapper kutoka Afrika Kusini, wameunganishwa kwenye collabo ya pamoja kwenye msimu mpya wa Coke Studio version ya Afrika Kusini.
Jumanne hii Wawili hao wameingia studio jijini Johannesburg kurekodi wimbo wao. Hii itakuwa ni mara ya tatu Diamond anashiriki kwenye kipindi hicho baada ya kushiriki mara mbili kwenye Coke Studio Africa inayofanyika jijini Nairobi, Kenya.
Akipost picha akiwa na Cassper, Diamond ameandika: Creating an Anthem in Coke Studio South Africa with my Hommie @casspernyovest now! #CokeStudioZa.”
Hasimu wa Cassper, AKA naye yupo kwenye msimu huu ambapo collabo yake amefanya na msanii wa Nigeria, Patoraking.
TAZAMA PICHA ZAIDI
Post a Comment