Header Ads

TZ HATUNA 'MADIRECTOR' WAKALI WA VIDEO- HANSCANA

Muandaaji wa muziki wa kizazi kipya nchini (Director) Hanscana amesema hapa nchini bado hakuna kampuni nzuri zaidi ya tano ambazo zinafanya vizuri katika kuandaa muziki jambo ambalo linafanya watu kuamini kampuni chache katika utendaji wa kazi.


Muandaaji huyo ameyasema hayo katika kipindi cha E News kinachorushwa na EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa ambapo amesisitiza umuhimu wa kuwa na kampuni nyingi zaidi zenye uwezo wa kutoa kazi zinazoendana na wakati wa sasa.
''Watu wanaotaka 'kushoot' video ni wengi sana nchini lakini watu ambao wana uwezo wa kutengeneza video kali ni wachache sana jambo ambalo linafanya kutokuwepo kwa mgawanyo wa kazi''-Amesema Hanscana

Aidha Muandaaji huyo wa muziki nchini amesema yeye biashara ndiyo inayoonyesha yupo 'level' gani katika kuaminika na kufanya kazi nzuri na wasanii mbalimbali.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.