SITAKI MNIFOLLOW KWENYE PAGE YANGU - TUNDA
Mrembo ambaye anafanya poa kwenye video za bongo Tunda, amewataka mashabiki wake kuwa wakweli na kuacha unafiki, la sivyo wamuache kumfuata kwenye mtandao wa kijamii.
Akiongea kwenye kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Television, Tunda amesema anachukizwa na kitendo cha watu kujadili mambo yasiyowahusu, pamoja na kuoneana wivu, na kuwataka wasimfollow kwenye mitandao ya kijamii.
"Wanaonipenda wanipende na wasionipenda waachane na mimi wasinifollow na kunijazia coments za kipumbavu pumbavu, ila wanaonipenda wanifollow", alisema Tunda.
Pia Mlimbwende huyo ambaye ana mahusiano na msanii wa muziki wa bongo fleva Young Dee, amesema anashangazwa na tuhuma anazopewa za kutumia madawa ya kulevya, na bado analifanyia utafiti suala hilo.
"Kitendo cha kuniambia natumia unga mpaka leo sijui limeanzia wapi, hata sijui ila naendelea kufuatilia" alisema Tunda.
Kwa sasa mrembo huyo ameamua kurudi shule baada ya kuacha kwa muda mrefu na kujihusisha na sanaa
Post a Comment