Header Ads

SUGU: SHOO YANGU YA KWANZA NILILIPWA TSH MILIONI 5


Kupitia kipindi cha Sun rise cha Times fm Sugu amesema shoo ambayo aliwahi kulipwa pesa nyingi ilifanyika mwanza alilipwa milion 5 hamkumbuki promota wa show hiyo lakini ana furahi kuona sasa show zina lipa vizuri, pia amemsifia Diamond kwa harakati zake japo yeye sio muumini wa muziki wa dizaini yake lakini anafurahi kuona mtu anafanya harakati na harakati zina mpa faida.


Amesmea moja ya harakati alizozifanya ni kupigania wasanii kulipwa pesa nzuri wakati wa kufanya show akatoa mfano msanii wa nje akija Tanzania anapata hela nzuri yule wa Tanzania ana pewa laki nne lakini amelipigania hadi sasa wasanii wamenufaika ametoa ushahidi kuwa hata ukifuatilia hotuba zake zilizo pita bungeni.


Sugu amesema kwa wale wote wanotaka kwenda ulaya inatakiwa wajipange na wawe na jambo maalumu wanalo enda kulifanya  bila yahivyo wataumia sana na hii sio ulaya bali hata sehemu yoyote nje ya nchi. hapa amewalenga wale wanao amini kuwa fursa zina patikana endapo wana enda nje ya nchi pasipo kuwa na jambo la kufanya.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.