Header Ads

TAIFA STARS KUREJEA USIKU WA MANANE



NA YOUNG

MASHUJAA wa kikosi cha timu ya soka taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’, wanatarajiwa kuwasili nchini Alfajili ya kesho wakitokea nchini Chad, walipokwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya timu hiyo ya taifa na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Stars, ilikwenda nchini humo kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya kutafuita nafasi ya kushiriki Mataifa Afrika nchini Gabon, 2017.

Taarifa iliyotumwa na Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, ilisema kuwa kikosi hicho kinatarajiwa nyumbani kesho usiku kwa usafiri wa shirika la ndege la Ethiopia.

Taarifa ya Kizuguto, ilisema Stars, itatoka N’Djamena Chad saa 8 mchana wa leo kupitia Addis Ababa na kasha, itafika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNIA) saa 7 usiku.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.