Alisema akiwa chooni anajiandaa kuoga, uchungu ulikata ghafla na baada ya dakika chache aliona kitu kinaning’inia sehemu za siri kisha kikadondoka chini.
Baada ya kuona hivyo, alianza kupiga kelele akiita “nesi, nesi” na ndipo alipopita wa kwanza ambaye hata hivyo hakumshughulikia na badala yake akaendelea na kazi zake, lakini baadaye akaenda daktari ambaye hakumtambua kwa jina, akamsaidia. “Nikiwa ninatapatapa sielewi alikuja daktari akamuokota mtoto ambaye alikuwa ameanguka chini karibu na tundu la choo,” alisema.
Baadhi ya wauguzi walitoa ushuhuda wa tukio hilo, wakiwamo daktari aliyemuokoa mama huyo na mwanaye chooni, lakini hawakutaka majina yao yatajwe gazetini. “Nilikuwa wodini. Wakati napita nikasikia mtu anapiga kelele chooni akiita ‘nesi, nesi, mwanangu jamani’. Nilishtuka, ikabidi niende kuona ndipo nikamkuta huyo binti akiwa amesima na kondo likiwa limening’inia na kitoto kichanga kimeanguka chini,” alisema.
Alieleza kuwa alikiokota kichanga hicho na mama yake kisha kuwapa huduma ya kumsafisha mtoto.
Muuguzi mwingine ambaye alikuwa zamu mchana, alisema alipopita kumuangalia mtoto huyo, alikuta akiwa na uvimbe kwenye paji la uso. “Nikamuuliza mama wa mtoto ndipo akanisimulia. Kwanza nikashangaa huyu nesi ilikuwaje akamruhusu mama ambaye anataka kujifungua kwenda chooni?” alihoji.
Mkuu wa Idara ya Wazazi, Grace Massawe alisema wamelichukua suala hilo na kwamba watalishughulikia.
Post a Comment