HARMONIZE ADAI KWAMBA AWEZI KUMKIMBIA HUDDAH MONROE.
Msanii ambaye kwa sasa ameanza kufanya vizuri na wimbo wake mpya 'Bado' Harmonize amefunguka na kusema hawezi kumkimbia Huddah Monroe
ikitokea wakakutana na kuachwa pamoja ndani ya chumba kimoja.
Kupitia kipindi cha Friday Night Live mtangazaji wa kipindi Sam Missago alimuuliza Harmonize kuhusu tetesi za wawili hao kutoka kimapenzi, ndipo aliposema kuwa si mpenzi wake japo wamewahi kukutana na Huddah Monroe kwa ajili ya kazi.
"Niliwahi kutana nae kwa ajili ya kazi lakini siyo kweli kwamba nilimkimbia tukiwa wawili ndani, Missago naanzaje kwa mfano kumkimbia mtoto mzuri kama yule eehh? Alihoji Harmonize
Katika hatua nyingine Harmonize anashukuru kwa uongozi wake wa WCB Wasafi kwani anadai umemsaidia kubadili maisha yake na kutumiza ndoto zake za kuwa msanii mkubwa.
"Unajua si vyema kusema kwa watu nimepata nini na nini ila nashukuru uongozi wangu wa Wasafi kwani umebadili maisha yangu saizi mimi naweza kuiangalia familia yangu, nimekutana na wasanii wakubwa na watu wazito kwa sababu ya Wasafi, lakini pia kama unavyoona nina uwezo wa kubadili nguo na vitu kama hivyo" Alisema Harmonize.
Post a Comment