EVENTS ;- WASHINDI WA PICHA BORA ZAIDI WATANGAZWA
Washindi na waliochukua nafasi ya pili katika tuzo za wapiga picha za Sony wametangazwa.
Washindi na waliochukua nafasi ya pili katika tuzo hizo wametangazwa ambapo Stefan Thaler ndio mshindi wa Austria na picha yake alioipiga huko Thierse,Tyrol
Washindi na waliochukua nafasi ya pili katika tuzo hizo wametangazwa ambapo Stefan Thaler ndio mshindi wa Austria na picha yake alioipiga huko Thierse,Tyrol
- Jopo la wataalam lilichagua picha nzuri iliopigwa na kuiorodhesha katika orodha ya picha bora za Sony mwaka 2016.Mohammed Ponir Hossain alikuwa wa pili kutoka Bangladesh
- tangu uzinduzi wake mwaka 2012,tuzo hizo za kitaifa imekuwa kutoka ushirika wa mataifa manane hadi sitini.Picha nzuri ya grafiki iliopigwa na Luis Portelles ilichukua nafasi ya tatu.
- Miguel Angel Merino Tapia kutoka Chile alichukuwa nafasi ya pili kwa picha yake ya kiwavi wa kwanza msimu huu,karibu na nyumba yake huko Puerto Montt
- Wang LiJun kutoka Uchina alichukua nafasi ya tatu.''Hitting Tree Flowers'' ni neno linalotumiwa kuelezea utamaduni wa Mkoa wa He Bei
- Kuwapiga ndege aina ya kulea ndio kitu ninachopenda sana,sichoki kufanya hivyo.Ni ndege maalum,alisema Petar sabol ambaye ndiye mshindi kutoka taifa la Croatia
- Victor Vargas alikuwa mshindi wa Ecuador na picha ya Volcano katika mlima wa Andes,uliofukiwa na jivu wakati wa mwezi mwekundu mnamo tarehe 27 mwezi Septemba 2015.
- Nader Saadallah kutoka Misri alikuwa wa pili na picha yake iliopigwa katika maonyesho ya Lijang ambayo yanaonyesha maisha na tamaduni za Naxi,yi bai huko Lijiang China
- Abhijit Banerjee kutoka India alikuwa mshindi na picha yake kwa jina Gangasagar,iliopigwa katika maonyesho makubwa zaidi nchini India ambayo hufanyika mashariki mwa kisiwa cha mji wa Bengal Sagar
- Hendra Permena,aliyeorodheshwa katika orodha ya tabasamu alikuwa wa pili kutoka Indonesia
- Mshindi wa Malaysia alikuwa Khairel Anuar Che Ani ambaye alipiga picha wakati ambapo wacheza densi wa Rejaang walikuwa wakingoja wakati wao kuingia ukumbini katika maonyesho mjini Bali
- Silvia Andrade kutoka Mexico ndio mshindi aliyepiga picha ya ulimwengu wa asili na picha ya mbegu inayokuwa.
- Pedro Diaz Molins ndio mshindi wa nafasi ya kwanza nchini Uhispania akiwa na picha ya wanandoa wazee katika ufukwe wa bahari.
- Mike O'Dwyer alichukua nafasi ya pili katika tuzo hizo kwa picha yake ya gwaride la wanajeshi wanamaji wa Uingereza wakati wa uzinduzi wa meli ya P&O Britannia
- Mshindi wa Vietnam ni Minh Thanh Ngo,aliyepiga picha ya utamaduni wa kuwasha taa za koroboi k atika mto Perfume mjini Hue
Post a Comment