Header Ads

BEN POL APATA MTOTO

10932191_1545721332379090_380810471_n
Benard Paul ‘Ben Pol’

MKALI wa Bongo Fleva, Benard Paul ‘Ben Pol’ amebahatika kupata mtoto wa kiume aliyezaa na mwandani wake wa siku nyingi anayefahamika kwa jina la Latifa, japo hakuwa tayari kuweka wazi kwa madai kuwa muda bado haujawadia.
Ishu hiyo iliyokuwa gumzo mwanzoni mwa wiki hii baada ya mwandani wake huyo kuposti picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akifurahia kupata mtoto wa kiume na kuainisha kuwa msanii huyo ndiye baba wa kachanga hako ndipo paparazi wetu alimtafuta Ben Pol ambaye aliweka msimamo kuwa muda ukifika ataweka wazi.
“Nashukuru kwa kupata mtoto, lakini hili jambo bado sijaamua kuliongelea japo siyo siri kwa sasa watu wengi wananipigia simu kunipongeza, yaani wamejua bila kutarajia ndiyo sababu hata kwenye mtandao sijaiweka hiyo ishu,” alisema Ben Pol.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.