EATV AWARDS, WAJUE WASHINDI WA TUZO NA ALI KIBA KUNYAKUA TUZO 3.
Mwanamuziki Alikiba ndiye msanii aliyejishindia tuzo nyingi katika usiku wa Tuzo za EATV 2016 zilizofanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Alikiba akitoa neno la shukrani kwa mashabiki wake
Aidha msanii wa filamu Salim Ahmed aka Gabo Zigamba ameondoka tuzo mbili.
Wasanii ambao walifanya show usiku huo ni pamoja na Darassa, Billnass, Lady Jaydee, Barnaba, Vanessa Mdee, Shetta, Alikiba pamoja na Maurice Kirya.
List ya washindi wote wa EATV Award
1. Kipengele cha tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume 2016 kimekwenda kwa Ali Kiba.
2. Wimbo wa Aje wa Ali Kiba umeshinda tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka 2016.
3. Video ya wimbo wa Aje ya Ali Kiba imeshinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka 2016.
4. Kipengele cha tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike 2016 kimekwenda kwa Lady Jay Dee.
5. Tuzo ya Heshima inayotolewa kwa mtu/taasisi yenye mchango mkubwa katika sanaa ya Tanzania inakwenda kwa Dj Bonny Love.
6. Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka 2016 imekwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu ya Gabo Zigamba.
7. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume 2016 inakwenda kwa mwigizaji Salim Ahmed maarufu Gabo Zigamba.
8. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike 2016 inakwenda kwa mwigizaji Chuchu Hans.
9. Navy Kenzo wameshinda tuzo ya Kundi Bora la Muziki 2016.
10. Mwanamuziki Man Fongo ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora Chipukizi 2016.
Angalia picha za show pamoja na utoaji wa tuzo.
MWANAMUZIKI BORA WA KIKE
MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI
KUNDI BORA LA MWAKA
VIDEO BORA YA MWAKA " AJE "
WIMBO BORA WA MWAKA " ALI KIBA - AJE "
FILAMU BORA YA MWAKA - " SAFARI YA GWALA "
MUIGIZAJI BORA WA KIUME - " SALIM AHMED { GABO }
MUIGIZAJI BORA WA KIKE - " CHUCHU HANS "
TUZO YA HESHIMA - BONY LUV
CHECK FULL BY CLICKING HERE GO NOW !!!
Post a Comment