YEMI ALADE NA NOMZAMO MBATHA WAUGANA NA BONANG MATHEBA KUSHEREHESHA TUZO ZA " MTV MAMA ".
Mastaa watatu wa Afrika akiwemo Bonang Matheba, Yemi Alade na Nomzamo Mbatha wanatarajiwa kusherehesha tuzo za MTV MAMA Jumamosi hii ya Oktoba 22.
“Serving us all the #BlackGirlMagic. MAMAnation, we give you the ladies that will host an epic #MTVMAMA2016.
@bonang_m @yemialade @nomzamo_m,” wameandika waandaaji wa tuzo hizo kwenye mtandao wao wa Instagram.
@bonang_m @yemialade @nomzamo_m,” wameandika waandaaji wa tuzo hizo kwenye mtandao wao wa Instagram.
Awali mchekeshaji wa Afrika Kusini anayeishi nchini Marekani, Trevor Noah alitangazwa kuwa mshereheshaji kwenye tuzo hizo lakini kupitia mtandao wake wa Twitter Ijumaa hii alithibitisha kutoshiriki kwenye tuzo hizo kwa madai kuwa ana matatizo ya sauti hivyo ameshauriwa na madaktari wake apumzike.
Tuzo hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome, Johannesburg, Afrika Kusini.
Post a Comment