Video: Ray C KURUDI KWENYE MUZIKI KWA KISHINDO CHA AINA YAKE.
Rehema Chalamila, how I wish arudi tena kwenye chati kama zamani. Ray C – kama unavyomjua zaidi, amepitia mapito mengi, na tena yaliyojaa njia yenye mbigili ibakishayo maumivu mguuni.
Miaka minne iliyopita, kwa hali aliyokuwa nayo, kila mtu alimkatia tamaa kuwa ndio basi tena ameshatumbukia kwenye shimo waliloshindwa kutoka vijana wengi. Matumizi ya madawa ya kulevya yalimuongezea jina la uteja lililolifunika jina lake la utani ‘kiuno bila mfupa.’ Rehema, msichana mrembo aliyekuwa ndoto ya wanaume wengi, akapoteza thamani yake.

Post a Comment