Header Ads

BARAKAH DA PRINCE , ALI KIBA & LADY JAY DEE WAJIUNGA * ROCK STAR4000 *


Hitmaker wa Siwezi, Barakah Da Prince amesainishwa mkataba wa usimamizi na kampuni ya Rockastar4000.

Ameungana na Alikiba na Lady Jay dee kuwa msanii wa tatu kuwa chini ya uongozi huo. Na kwa sasa muimbaji huyo atakuwa akijulikana kama ‘ Barakah The Prince.’

Kwenye maelezo yake, CEO na mwanzilishi wa label hiyo, Jandre Louw amedai kufurahishwa kumsaini muimbaji huyo wa Mwanza na kumwelezea kama mwenye kipaji cha hali ya juu.




Akiwa chini ya label hiyo, Barakah ataanza kuandaa album yake ya kwanza itakayotoka mwaka 2017.Muimbaji huyo amejipatia umaarufu kwa nyimbo zake kama Siachani Nawe, Nivumilie na Siwezi.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.