Header Ads

MABESTE ;- SIJAFIKIRIA KUTENGENEZA ALBAMU KWA SASA.


MKALI wa Bongo Fleva, Mabeste Venance ‘Mabeste’ amefunguka kuwa kutokana na mfumo wa uuzaji albamu ulivyo hapa Bongo unamnyima fursa ya kufikiria kutengeneza albamu ya nyimbo zake.
Mkali huyo anayetamba na ngoma kama Dole, Baadae Sana, Sukuma na nyingine nyingi, ameenda mbali zaidi na kusema si kwamba wasanii wengi wa Kibongo kukosa fursa ya kutengeneza albamu kutarudisha nyuma soko la muziki wa hapa nyumbani, bali njia zipo nyingi za kutoboa.
“Binafsi sijafikiria kutengeneza albamu kwa sasa kutokana na mfumo wa uuzaji wake ulivyo hapa Bongo, wasanii wengi wanaotengeneza albamu wanajisimamia wenyewe katika kutafuta masoko ya kwenda kuuzia, wapo ambao wanapata hasara kubwa na wengine wanafaidika kidogo.
“Nitaendelea kutengeneza ngoma hadi ngoma na muda ukifika wa kufanya hivyo nitafanya, kikubwa ninachotaka kusema ni kwamba hali hii haiwezi kulifanya soko la muziki hapa Bongo kushindwa kupasua, tuatendelea kujitangaza kupitia staili hizi kwani njia ni nyingi za kufanikiwa bila hata albamu kama wafanyavyo mataifa ya mbele,” alisema Mabeste ambaye ‘soon’ ataibariki ndoa yake na mama mtoto wake, Lisa Karl Fickenscher.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.