Header Ads

LADY JAY DEE AMTAMBULISHA MUME WAKE KWENYE TUZO ZA EATV AWARDS.

Msanii mkongwe wa muziki Lady Jay Dee ameutumia usiku wa EATV Awards 2016 kumtambulisha rasmi mbele ya mashabiki mwanaume ambaye anadaiwa kuwa ni mume wake.

lady-jay-dee
 
Lady Jay Dee akipongezwa na mume wake
Muimbaji huyo ambaye usiku jana aliambatana na mwanaume huyo kupokea tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike, alilitumia jukwaa hilo kuwashukuru mashabiki wa muziki wake pamoja na kumtambulisha mwanaume huyo ambaye ni mgeni machoni pa wengi.
Baada ya shukrani kwa mashabiki na kutaka kuondaka alirudi jukwaani nakusema, “Nilitaka kusahau huyu ni baby wangu” kauli ambayo iliibua shangwe kubwa kwa mashabiki.
Wiki chache zilizopita, muimbaji huyo kupitia Instagram alipost picha ya mwanaume huyo na kuandika:

“Big shout out kwa Coastal air Kwa kufanikisha safari yangu kwenda honeymoon #ZanzibarIsland,”
kauli ambayo ilitafsiriwa huwenda wawili hao wamefunga ndoa.
Jay Dee hakuwahi kuweka wazi mahusiano yake tangu aachane na aliyekuwa mue wake, Gardiner G Habash.

2 comments:

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.