PROF JAY AZIDI KUTATUA KERO MIKUMI

Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro Joseph Haule amefanikiwa kupunguza tatizo la maji kwa wakazi wa jimbo hilo kwa kuchimba Kisima kikubwa kitakachowawezesha wakazi wa Mikumi kupata maji yaliyo safi na salama.
Mh Haule amesema kuwa amelazimika kuchimba kisima hicho ili kupunguza tatizo la maji wakati wakiendeleaa kutathmini namna nzuri zaidi ya kusambaza mabomba na kumaliza kabisa tatizo la maji katika mji mdogo wa Mikumi.

Post a Comment