Header Ads

NDANDA FC YAJICHIMBIA MOROGORO KUIWINDA YANGA

Uongozi wa Timu ya Ndanda FC umesema wanaamini wanauwezo wa kuchukua pointi tatu mbele ya Yanga katika hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho na kuwawezesha kusonga mbele katika michuano hiyo.
Afisa habari wa Ndanda FC Idriss bandari amesema, kikosi kipo kambini Mkoani Morogoro kwa ajili ya kambi ya takribani siku saba kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Bandari amesema, mchezo dhidi ya Yanga ni mgumu na hawajawahi kupata matokeo mazuri zaidi ya sare hivyo wanaamini kikosi kitacheza vizuri ili kuhakikisha kinapata matokeo mazuri katika mchezo huo.
Bandari amesema, kila mchezaji anajua jukumu lake awapo Uwanjani hivyo wanaamini ushirikiano na akili ya kila mchezaji itaiwezesha timu hiyo kuweza kupata pointi tatu zitakazowawezesha kuweza kusonga mbele katika hatua ya nusu Fainali ya michuano hiyo.

No comments

YoungGskillz.com . Powered by Blogger.