Moja ya malalamiko mengi ya bendi za muziki hapa bongo ni kukosa #Airtime kwenye media za bongo. Kilio hiki hakupo kwa bendi ya Yamoto kutoka mkubwa na wanawe ambao wametoa tofauti kubwa zinazowaweka mbali na janga la kukosa promo.
Mmoja wa wasanii wa kundi hilo,Aslay amesema sababu kuu ni kuwa kwanza wanatunga nyimbo fupi fupi tofauti na za bendi nyingine.Pili aina ya muziki wao una ladha za #bongofleva ambazo zinapendwa na wengi.
Jingine wamesema hata muonekano wao wawapo stejini ni Siri nyingine . Kwasasa Yamoto ambao wanatamba na wimbo wao #Mama ft zena wamemuongeza msanii mmoja kutoka kundi LA salam kwahiyo Yamoto watakuwa 5.
Post a Comment