Muonekano wa unamaana kubwa sana kwa msanii hasa kibiashara, pia muonekano huo humtofautisha msanii na watu wengine jambo ambalo lina wafanya mashabiki wake kuvutiwa, msanii Tunda Man aliwahi kufungukia suala la wasanii kulipwa mkwanja mdogo kwenye show na kueleza kuwa muonekano ndio hupelekea msanii kulipwa vizuri.
Kwa upande wake Hit Maker wa My Life Dogo Janja amefunguka juu ya muonekano wake mpya na kueleza kuwa hapo awali alikuwa na muonekano wa kawaida ambao ulimfanya atangeneze mashabiki wengi wa uswahilini hivyo anaimani kwa muonekano wake mpya ataweza kuingia sehemu yeyote na kutengeneza mashabiki wa aina mbalimbali.
Akizungumzia ujio wake mpya na ngoma yake ya My Life Dogo Janja amesema kuwa amepania kama msanii anaetaka kutoka hivyo amejipanga kwa nyimbo nyingi zenye kukonga nyoyo za mashabiki wake hivyo amewataka wakae mkao wa kula kwa kazi hizo.
Post a Comment