Baada ya mwanadada Gigy Money ambaye ni Video Queen wa vichupa hapa Bongo kuweka wazi kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na Rich Mavoko,hatimaye msanii huyo ameamua kulifungukia suala hilo na kusema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi na Gigy Money
Kupitia kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na EATV Gigy alisema Rich Mavoko alishawahi kugombana na Hemedy kisa yeye jambo ambalo Rich Mavoko amelikanusha na kutaka Hemedy PhD aulizwe kama ni kweli walishawahi kugombana.
Rich Mavoko amesema hakumbuki kama alishawahi hata kukutana na Gigy Money na hadi sasa hajui kilichosababisha kuongea maneno hayo ambayo hayana ukweli hata kidogo.
Ameongeza kuwa yeye siyo mtu wa kupenda skendo za kipumbavu kama hizo na hamjui huyo Gigy Money wala hajawahi kumuona na siyo habari anazotaka kuziongelea tena.
Post a Comment