RAY ASEMA KWAMBA MAJI NA MAZOEZI YAMFANYA KUWA MWEUPE.

Staa wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ baada ya kudai kuwa weupe wake unatokana na kunywa maji mengi na kufanya mazoezi na siyo mkorogo, makampuni manne yanayojishughulisha na masuala ya maji yamemtaka awe balozi wao.
Ray
Akizungumza na gazeti la Mtanzania jana, Ray alisema kubadilika kwake kwa ngozi kumeleta gumzo kubwa kwake na pia kumempatia neema kutokana na makampuni hayo kutaka awe balozi wao.
“Kunywa kwangu maji kwa wingi na kushiriki mazoezi ipasavyo ndiyo kumepekekea ngozi yangu kuwa nyororo na makampuni yaliyojitokeza kwa sasa nimewaambia wasubiri kwanza hadi nitakapokuwa tayari kuwa balozi wao,’’ alieleza Ray.
RAY ASEMA KWAMBA MAJI NA MAZOEZI YAMFANYA KUWA MWEUPE,,,,,,,,ME NA WE HATUJUI EBU TUJARIBU,
Post a Comment