G20;- KUONDOKA KWA UK KUTAATHIRI UCHUMI DUNIANI
Mawaziri wa fedha kutoka mataifa yaliyostawi duniani wameonya kuwa uchumi wa dunia utaathirika ikiwa Uingereza itaamua kuondoka kutoka kwa muungano wa ulaya wakati wa kura ya maoni ya mwezi June.
Matamshi hayo yanajumuishwa katika taarifa iliyotolewa katika taarifa ya mwisho kwenye mkutano wa siku mbili wa mataifa ya G20 mjini Shanghai.
Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ambaye anataka nchi yake kubaki Ulaya aliambia BBC kuwa hakutaka hilo kutamkwa wakati wa taarifa ya mwisho.
Mawaziri wa mataifa ya G20 wanasema kuwa ukuaji wa uchumi ulikuwa wa chini kuliko ilivyotarajiwa.
Post a Comment